Baada ya jana kutoa asisti ya goli la pili la Hugo Ekitike kwenye ushindi wa 2-0 wa Liverpool dhidi ya Brighton, Mohamed Salah sasa amekuwa mchezaji wa tatu kwa wachezaji waliochangia mabao mengi wa muda wote wa Ligi Kuu Uingreza, akiwa amewapita Frank Lampard na Ryan Giggs huku akiwa amechangia mabao 280 (Magoli 190, Assists 90).
Wachezaji wawili walio mbele yake ni Alan Shearer na Wayne Rooney.
1 Alan Shearer 324
2 Wayne Rooney 308
3 Mohamed Salah 280
4 Frank Lampard 279
5 Ryan Giggs 272
Salah alifanikisha hatua hii katika michezo michache zaidi kuliko wachezaji wengine katika tano bora, akiangazia ufanisi wake wa ajabu.
Pia anashikilia rekodi ya kuhusika kwa mabao mengi zaidi katika msimu mmoja wa mechi 38 za Ligi Kuu, akiwa na mabao 47 msimu wa 2024/25.










Leave a Reply