Home KITAIFA SIMBA YAKATAA UHUNI KWENI KWENYE MPIRA WA MIGUU

SIMBA YAKATAA UHUNI KWENI KWENYE MPIRA WA MIGUU

528
0
simba

UONGOZI wa Simba SC umeweka wazi kuwa haukubaliani na vitendo vya kihuni kwenye mpira wa miguu kwa kuwa unarudisha nyuma maendeleo ya wachezaji na timu kiujumla.

Simba SC inapeperusha bendera katika Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa hatua ya pili inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kimataifa dhidi ya Nsiginzini Hotspurs Oktoba 19 2025 pia inaongoza ligi ikiwa na pointi sita baada ya mechi mbili.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa vitendo vya kihuni ambavyo vinatokea uwanjani kwa wachezaji kuchezeana rafu mbaya vinaumiza wachezaji na kudumaza maendeleo ya mpira kutokana na wachezaji kukaa nje muda mrefu wakipambania hali zao.

“Vitendo vya kihuni kwenye mpira wa miguu havifai kwa kuwa vinadumaza maendeleo ya mpira na sio mpira tu hata maendeleo ya mchezaji husika yanadumaa kwa kuwa maisha yake yapo kwenye mpira hapo anaendeleza maisha na familia.

“Inapotokea mchezaji mwingine anamchezea faulo mbaya mchezaji hii inamaana kwamba anahatarisha maisha yake na maisha ya familia yake. Wapo wachezaji ambao wamekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu na hii imetokana na kufanyiwa vitendo vya kihuni.

“Muhimu kila mchezaji kuwa mlinzi wa mchezaji mwengine hili litafanya mpira usiwe wa kihuni na rafu mbaya hazifai kwa kuwa mpira ni maisha na maisha yanatengenezwa kila hatua ambayo inapigwa.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here