Home KITAIFA YANGA SC MWENDO WA TUNAPIGA KICHWANI TU

YANGA SC MWENDO WA TUNAPIGA KICHWANI TU

75
0
wiki ya wananchi yanga

JIUNGE KWENYE WHATSAPP CHANNEL YA SIMULIZI ZA SAUTI ZA WAKUBWA TU BONYEZA HAPA KUJIUNGA

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC ameweka wazi kuwa kwa sasa Yanga SC hakuna suala la kupeana matumaini bali ni mwendelezo wa dozi pale ambapo waliishia.

Ipo wazi kwamba Yanga SC ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuelekea msimu mpya wa 2025/26. Kwa sasa wana jambo kubwa la Wiki ya Mwananchi ambalo linatarajiwa kufanyika Uwanja wa Mkapa Septemba 12 2025.

Yanga SC itacheza mchezo wa kirafiki na Klabu ya Bandari ya Kenya na kwa sasa wanaendelea na hamasa kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi na slogan yao inasema Tunapiga Kichwani Tu.

“Wanayanga sasa wamevuka level ya kuwa na Slogan za kupeana matumaini, tumekubaliana huu ni msimu wa vitendo na tumegundua watu bado wanataka dozi, kuanzia sasa tunaenda kupiga kichwani tu. Hiyo ndio slogan yetu, Tukipiga kichwani tunacheza na ufahamu. Mwaka huu ni kichwa tu, tumeweka kabisa nyundo kwa ajili ya wale wanaokaza fuvu.

“Kwa upande wa tiketi, mashabiki wa Yanga SC waendelee kukata tiketi kwa kuwa kila kitu kinakwenda sawa.Kulikuwa na changamoto mwanzo lakini kwa sasa kila sehemu wapo wanaouza tiketi. Na ukiona mwamvuli wenye nembo ya Wiki ya Mwananchi wewe kata tiketi.”

Katika uzinduzi wa Wiki ya Mwananchi, Septemba 3 2025 Mbagala, mashabiki wengi wa Yanga SC walijitokeza na kulikuwa na burudani kali kinomanoma siku hiyo na sasa zinahesabiwa siku kabla ya tukio lenyewe kukamilika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here