Home KITAIFA RASMI HII HAPA TAREHE YA SIMBA DAY 2025

RASMI HII HAPA TAREHE YA SIMBA DAY 2025

298
0

Uongozi wa klabu ya Simba SC umetangaza rasmi kuwa Septemba 10, 2025 itakuwa siku ya kufanyika kwa Simba Day, tamasha kubwa barani Afrika linalotumika kwa ajili ya kuwatambulisha wachezaji wapya, wachezaji waliopo pamoja na benchi la ufundi kuelekea msimu mpya wa 2025/26.

Kwa sasa, kikosi cha Simba SC chini ya Kocha Mkuu Fadlu Davids kipo kambini nchini Misri, kikiendelea na maandalizi ya msimu mpya.

Msimu uliopita, Simba SC ilionyesha ushindani mkubwa kwenye anga la kimataifa baada ya kufika hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo ilimaliza ikiwa nafasi ya pili nyuma ya RS Berkane. Vilevile, kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC, Simba ilikamilisha msimu ikiwa nafasi ya pili, ligi inayotajwa kuwa ya nne kwa ubora barani Afrika.

Advertisement

Miongoni mwa wachezaji wapya walioungana na kikosi cha Simba SC ni:

  • Jonathan Sowah, mshambuliaji kutoka Singida Black Stars, aliyefunga mabao 13 msimu uliopita.
  • Anthon Mligo, beki wa kushoto aliyejiunga akitokea Namungo FC.
  • Naby Camara, beki aliyeongeza nguvu katika safu ya ulinzi.

Kwa upande mwingine, baadhi ya nyota hawatakuwa sehemu ya kikosi kipya cha Simba SC. Wachezaji waliotajwa kuondoka ni pamoja na:

  • Mohamed Hussen Zimbwe Jr, ambaye ametua Yanga SC kwa kandarasi ya miaka miwili.
  • Aishi Manula, aliyesajiliwa na Azam FC baada ya muda mrefu akihudumu Simba.

Mashabiki wanatarajia burudani kubwa na utambulisho wa aina yake katika Simba Day, siku ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikihusisha muziki, burudani na sherehe kubwa za michezo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here