Home KITAIFA MOROCCO KUKUTANA NA MOROCCO, KIVUMBI CHAN 2024

MOROCCO KUKUTANA NA MOROCCO, KIVUMBI CHAN 2024

67
0

TIMU ya Taifa ya Tanzania inayofundishwa na Kocha Mkuu, Hemed Suleman maarufu kwa jina la Morocco itacheza na timu ya taifa ya Morocco kwenye mchezo wa robo fainali CHAN 2024 Uwanja wa Mkapa.

Tanzania inaongoza kundi B ikiwa na pointi 10 baada ya mechi nne ambapo katika mechi hizo ilipata ushindi mechi tatu na kugawana pointi mojamoja kwenye mchezo mmoja Uwanja wa Mkapa.

Agosti 22 2025 wababe hawa wanatarajiwa kukutana Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Advertisement

Ikumbukwe kwamba Morocco ilikuwa Kundi A imegotea nafasi ya pili ikiwa na jumla ya pointi 9 baada ya kucheza jumla ya mechi nne katika CHAN 2024. Vinara wa kundi A ni  Kenya iliyokusanya jumla ya pointi 10 sawa na Tanzania.

Morocco ambaye ni kocha wa Tanzania aliweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa hatua ya robo fainali na wanatambua kila kundi lilikuwa na timu ngumu.

“Kila kundi lilikuwa na timu ngumu hivyo hatuna mashaka na mpinzani wetu. Niliwatazama Kenya, Morocco kila kundi.Kwenye hii michuano hakuna timu nyepesi. Tupo tayari kwa ajili ya kupambana na wachezaji wanatambua hatua inayofuata ni ngumu zaidi.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here