Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » CLEMENT MZIZE KUKOSEKANA KWA MIEZI MIWILI YANGA SC
    KITAIFA

    CLEMENT MZIZE KUKOSEKANA KWA MIEZI MIWILI YANGA SC

    ChikaoBy ChikaoNovember 6, 202501 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    mzizee yanga sc
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    Mshambuliaji wa Yanga SC, Clement Mzize, ataukosa mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC FC utakaopigwa Novemba 9, 2025 saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa KMC Complex, kutokana na majeraha ya goti.

    Mzize, ambaye amefanyiwa upasuaji wa goti lililokuwa likimsumbua kwa muda mrefu, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki nane hadi kumi, hali inayomfanya kukosa michezo kadhaa muhimu ya ligi.

    Nyota huyo pia alikosekana katika mchezo uliopita ambapo Yanga SC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Oktoba 28, 2025 kwenye uwanja huohuo, mabao yakifungwa na Zimbwe Jr pamoja na Ecua.

    Kutokana na kukosekana kwake, mabingwa hao watetezi wameendelea kumtegemea mshambuliaji Prince Dube, ambaye bado hajaonyesha kiwango chake cha kilele tangu kurejea uwanjani. Dube alianza katika kikosi cha kwanza mchezo uliopita lakini alishindwa kukamilisha dakika 90.

    Yanga SC inaingia katika mchezo ujao dhidi ya KMC ikitafuta kuendeleza rekodi yake nzuri ya matokeo, huku benchi la ufundi likikabiliwa na jukumu la kuhakikisha pengo la Mzize halitahiri mwendelezo wa ushindi.

    Yanga SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleSIMBA KUANZIA NYUMBAN MECHI YA KIMATAIFA, DHIDI YA PETRO DE LUANDA
    Next Article Mikoa Yote Matokeo Ya Darasa La Saba 2025/2026 – NECTA Standard Seven Results (PSLE)

    Related Posts

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    April 8, 2026

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    April 7, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    MBAPPE: NITACHEZEA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.