HomeKITAIFAMO DEWJI AHOJI MAGEUZI SIMBA, GUMZO MTANDAONI

MO DEWJI AHOJI MAGEUZI SIMBA, GUMZO MTANDAONI

WAKATI uongozi wa klabu ya Simba ukiendelea kusukuma mbele ajenda ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji, mwekezaji na Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewji (Mo Dewji), ameibua sintofahamu kubwa baada ya kuhoji hadharani hatua iliyofikiwa katika mchakato huo, akionekana kutoridhishwa na mwelekeo unaochukuliwa.

Sintofahamu hiyo imejitokeza kufuatia Simba kusaini mikataba ya makubaliano na Mainstream Group pamoja na Nexus Pesa kwa ajili ya urejeshaji wa zoezi la usajili wa wanachama na utoaji wa kadi za uanachama kwa kuzingatia katiba ya klabu, kuanzia ngazi ya matawi hadi makao makuu.

Hata hivyo, wakati uongozi ukieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mageuzi yanayolenga kuimarisha uendeshaji wa klabu, Mo Dewji kupitia mtandao wa kijamii ameonekana kuvuta breki ghafla kwa kuuliza swali moja lenye uzito mkubwa, “Transformation mmefikia wapi?”

Swali hilo, lililoandikwa kwenye ukurasa rasmi wa Instagram wa Simba leo Februari 10, 2026, lilikuwa ni mchango wa Mo Dewji katika taarifa iliyokuwa ikimnukuu Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu, kuhusu kurejeshwa kwa usajili wa wanachama,  hatua iliyotarajiwa kuleta umoja lakini badala yake imefungua mjadala mpana.

Kauli hiyo ya Mo Dewji imezua tafsiri tofauti miongoni mwa Wanasimba, wengine wakiona kama ni ujumbe wa kuhoji uwazi wa mchakato wa mabadiliko, huku wengine wakitafsiri kama ishara ya kuwepo kwa tofauti za kimtazamo kati ya mwekezaji huyo na uongozi wa klabu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular