Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » KIUNGO KAGERA SUGAR, JKT TANZANIA MSHAMBULIAJI KUREJESHA KWA JAMII, MKUDE NDANI
    KITAIFA

    KIUNGO KAGERA SUGAR, JKT TANZANIA MSHAMBULIAJI KUREJESHA KWA JAMII, MKUDE NDANI

    ChikaoBy ChikaoJuly 2, 202502 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Mkudeee
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    KATIKA kurejesha kwa jamii wachezaji, Nassor Kapama ambaye ni kiungo wa Kagera Sugar pamoja na mshambuliaji wa JKT Tanzania, Mohammed Bakari ‘Muddy Beka’ Julai 12, mwaka huu wanatarajia kucheza mechi ya hisani ikiwa na lengo maalum la kusaidia watu wasiojiweza.

    Mechi hiyo imeeandaliwa maalum na nyota hao ambao wanashiriki Ligi Kuu Bara ambapo itafanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kigamboni, Dar huku kiasi chote ambacho kitapatikana katika mechi hiyo kitatolewa kwa wahitaji.

    Muandaaji wa mchezo huo, Kapama amesema, kuwa maandalizi ya mchezo huo hadi sasa yanaendelea ambapo lengo kubwa la kufanya hivyo ni kutaka kusaidia wanajamii wa eneo hilo.

    “Hadi sasa kila kitu kinaendelea vizuri kuhusiana na mchezo huu ambao lengo kubwa ni kurudisha kwa jamii ambayo tunakaa nayo lakini pia kutoa kile kidogo ambacho tunacho.

    “Fedha ambazo zitapatikana katika mchezo huu basi zitaenda kwa kundi hilo ambapo tunakaribisha watu na kampuni kuja kudhamini mchezo wetu huu ambao tunatarajia kutakuwa na mastaa mbalimbali wa ligi kuu.

    “Kwenye mechi yetu hii kutakuwa na timu ya Kapama na Timu ya Muddy Beka na baadhi ya mastaa ambao watakuwa sehemu ya mchezo huu ni Mkude (Jonas), Erasto Nyoni, Hassan Dilunga, Joash Onyango, Abdultwalib Mshery, Hussein Kazi, Abal Kassim na wengine zaidi tutawatambulisha kwa kila siku zinavyokwenda,” alisema Kapama.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleBEKI YANGA SC MKATABA WAKE UMEKWISHA, ATAJA ATAKAPOSAINI
    Next Article ALI KAMWE, ASHANGAZWA NA MAUNO YA BONGE LA DADA

    Related Posts

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    March 24, 2026

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    March 24, 2026

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    March 24, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    Yanga Yamrudisha Kocha Abdihamid Moalin Kuinua Kiwango cha Timu

    Zidane Kurithi Mikoba ya Deschamps Ufaransa Baada ya Kombe la Dunia 2026

    Katibu wa Senegal asema Kombe halitaondoka Nchini kwao.

    FIFA YAPITISHA SHERIA MPYA 6 KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2026

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.