Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » KIBABAGE KUIBUKIA RASMI SINGIDA BLACK STARS
    KITAIFA

    KIBABAGE KUIBUKIA RASMI SINGIDA BLACK STARS

    ChikaoBy ChikaoAugust 27, 202501 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    kibabage
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    ALIYEKUWA beki wa kushoto wa Yanga SC, Nickson Kibabage tayari amejiunga na Singida Black Stars kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya mara baada ya kuachana na timu hiyo, katika msimu ujao.

    Beki huyo alikuwa katika kikosi cha Yanga SC msimu wa 2024/25. Alitwaa taji la ligi chini ya Kocha Mkuu Miloud Hamdi ambaye kwa sasa hayupo ndani ya kikosi hicho.

    Timu hiyo inanolewa na Romain Folz ambaye ni raia wa Ufaransa kwa sasa wapo kwenye maandalizi ya msimu mpya 2025/26.

    Inaelezwa kuwa taratibu zote za uhamisho wa beki huyo aliyempisha Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ aliyejiunga na Yanga SC kwa mkataba wa miaka miwili ambaye kwa sasa atakuwa kwenye changamoto mpya.

    Kibabage hakuwa chaguo la kwanza msimu uliopita kwenye mechi 30 za ligi alipata nafasi ya kucheza jumla ya mechi 12 pekee msimu wa 2024/25.

    Katika mechi hizo 12 alikomba jumla ya dakika 889, hivyo huenda akawa kwenye changamoto mpya msimu ujao unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

    Ikumbukwe kwamba anarejea kwenye timu ambayo aliwahi kucheza kabla ya kujiunga na Yanga SC.

    Yanga SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleSIMBA SC WAWATULIZA WAARABU, MPANZU NA KIBU WACHEKA NA NA NYAVU
    Next Article CARABAO CUP: EVERTON, FULHAM, BRIGHTON NA MAN UNITED KAZINI LEO USIKU!

    Related Posts

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    March 24, 2026

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    March 24, 2026

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    March 24, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    Yanga Yamrudisha Kocha Abdihamid Moalin Kuinua Kiwango cha Timu

    Zidane Kurithi Mikoba ya Deschamps Ufaransa Baada ya Kombe la Dunia 2026

    Katibu wa Senegal asema Kombe halitaondoka Nchini kwao.

    FIFA YAPITISHA SHERIA MPYA 6 KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2026

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.