Home KITAIFA NEYMAR AMWAGA MACHOZI AKIKUTANA NA KIPIGO KIKUBWA ZAIDI KWAKE

NEYMAR AMWAGA MACHOZI AKIKUTANA NA KIPIGO KIKUBWA ZAIDI KWAKE

154
1
Neymar

Nyota wa Brazil na klabu ya Santos Neymar Jr usiku wa kuamkia leo alitoka uwanjani akimwaga machozi baada ya kukumbana na kipigo kikubwa zaidi kwenye maisha yake ya soka klabu yake ikikumbana na kipigo cha magoli 6-0 dhidi ya Vasco da Gama kwenye mchezo wa ligi kuu Nchini humo.

Akizungumza baada ya mchezo huo nyota huyo mwenye miaka 33 aliyejiunga na klabu hiyo ya nyumbani kwao mapema mwaka huu amesema amevunjika moyo na uchezaji wa timu yake.

“Ninajisikia aibu,nimevunjika moyo kabisa  na uchezaji wetu mashabiki wana kila haki ya kuandamana na wakitaka kulaani na kutukana wana haki hiyo” Amesema Neymar baada ya mchezo huo.

Advertisement

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here