MAHODHA wa Simba, Shomari Kapombe aibua gumzo baada ya kushindwa kuweka wazi maana halisi ya staili yake mpya ya kushangilia mabao, inayohusisha kutembea kama mzee anayesaidiwa na mkongojo, akisema ni staili atakayoendelea nayo kila anapofunga.
Kapombe alionekana kwa mara ya kwanza akitumia staili hiyo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Esperance de Tunis, uliochezwa hivi karibuni, ambapo alishangilia kwa namna iliyowaacha wengi njia panda.
Katika kushangilia huko, beki huyo wa kulia alionekana akishika mfano mkongojo, ishara iliyozua tafsiri tofauti miongoni mwa mashabiki, huku baadhi wakiamini ni ujumbe maalum aliokusudia kuuwasilisha.
Akizungumza kuhusu staili hiyo, Kapombe amesema ameamua kuitumia kama sehemu ya kujipa motisha binafsi, hasa kutokana na maneno ya kubezwa anayopata kutoka kwa baadhi ya watu.
Nahodha huyo wa Simba aliongeza kuwa kila atakapopata nafasi ya kufunga, ataendelea kushangilia kwa staili hiyo ya kutembea kama mzee, kama njia ya kuwajibu wanaomdharau au kumuita mzee.
“Hivi sasa nawaacha wanaoelewa maana yake waendelee kuelewa kwa njia yao, lakini hapo baadaye nitaweka wazi sababu hasa zilizonifanya nichague hii staili,” amesema Kapombe.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, staili hiyo ya Kapombe inalenga kuwapa majibu wale wanaomkosoa na kumbeza, huku akionyesha kuwa bado ana nguvu, ari na ‘damu inayochemka’ ndani ya uwanja.
Maelezo ya Makala (Body Content): Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amevunja ukimya na kumwagia sifa nzito kiungo wa zamani, Kagoma, kufuatia kiwango chake bora cha kuaminika katika safu ya ulinzi wakati wa mchezo dhidi ya Mashujaa FC uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Kagoma, amba
KOCHA Mkuu wa Simba, Steve Barker, amewasha moto wa mbio za ubingwa kwa kutangaza wazi dhamira ya kukifikisha kikosi chake kwenye ushindi wa tisa, huku akitoa onyo zito kwa wachezaji wake kutobweteka wala kuruhusu mafanikio ya awali kuwapunguzia makali katika Ligi Kuu Tanzania Bara. Barker ameweka w
Kinda hatari wa soka duniani, Lamine Yamal, ameendelea kuishangaza dunia baada ya kuweka rekodi ya kufikisha mchango wa mabao 20 (mabao 12 na pasi za mabao 8) ndani ya michezo 13 pekee ya msimu huu wa 2026/27, akiwa na klabu yake ya FC Barcelona pamoja na timu ya taifa ya Uhispania. Kasi hii ya kuti
Aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Yanga SC, Haji Sunday Manara, ametoa tahadhari kwa mashabiki na wanachama wa Yanga akieleza kuwa wapinzani wao Simba SC wameonyesha dhamira kubwa ya kutwaa mataji msimu huu baada ya kuichapa Mashujaa FC mabao 6-1. Manara amesema kiwango kilichoonyeshwa na Simba katika m