MOROCCO YAWASILI RASMI TANZANIA KUKABILIANA NA STARS CHAN 2024

Kikosi cha wachezaji pamoja na viongozi wa timu ya Taifa ya soka ya Morocco, inayofahamika kama ‘Simba wa Milima ya Atlas’, kimewasili Dar es Salaam kwa maandalizi ya mchezo wa robo fainali ya CHAN 2024 dhidi ya ‘Taifa Stars’ ya Tanzania.






