Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » SIMBA SC KUFANYA USAJILI MKUBWA KUELEKEA MSIMU MPYA
    KITAIFA

    SIMBA SC KUFANYA USAJILI MKUBWA KUELEKEA MSIMU MPYA

    ChikaoBy ChikaoJuly 18, 202502 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    KUELEKEA msimu mpya wa 2025/26, Simba SC wamebainisha kuwa watafanya usajili mkubwa kupata timu imara ya ushindani kitaifa na kimataifa.

    Ipo wazi kuwa Aishi Manula ambaye ni kipa huyu atakuwa ndani ya Azam FC, Omary Omary amepelekwa kwa mkopo Mashujaa FC, Fabrince Ngoma mkataba wake umeisha, Kelvin Kijili atakuwa ndani ya Singida Black Stars ni baadhi ya wachezaji ambao hawatakuwa ndani ya kikosi cha Simba SC msimu ujao.

    Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa wanakuja na kishindo. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 Simba SC ilipishana na mataji yote iliyokuwa ikisaka.

    Taji la Ngao ya Jamii ni Yanga SC walitwaa, taji la CRDB Federation Cup, Yanga SC walitwaa taji la Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC ni Yanga SC walitwaa huku lile la Kombe la Shirikisho Afrika ni RS Berkane ya Morocco walitwaa taji hilo.

    Ally amesema wanatambua kwamba ulikuwa ni msimu wenye ushindani hivyo Wanasimba wasiishiwe nguvu, mipango inapangwa na usajili unafanyika mkubwa kuelekea msimu mpya wa 2025/26.

    “Kwa sasa viongozi wa Simba SC wametapakaa kila kona kwenye nchi za Afrika kwa ajili ya kumalizia usajili wa wachezaji wapya. Huu ni usajili mwingine wa kishindo na sitaongea sana safari hii nitaacha watu waone wenyewe.”.

    Simba SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleYANGA SC YAMTAMBULISHA NYOTA WA KISHINDO CHA BILIONI 87
    Next Article VIPERS SC YAMSAJILI WINGA MNIGERIA ODILI CHUKWUMA KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI

    Related Posts

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    March 24, 2026

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    March 24, 2026

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    March 24, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    Yanga Yamrudisha Kocha Abdihamid Moalin Kuinua Kiwango cha Timu

    Zidane Kurithi Mikoba ya Deschamps Ufaransa Baada ya Kombe la Dunia 2026

    Katibu wa Senegal asema Kombe halitaondoka Nchini kwao.

    FIFA YAPITISHA SHERIA MPYA 6 KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2026

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.