KITAIFA

UBAYA UBWELA UWANJA WA MKAPA KITAUMANA

UBAYA ubwela itakuwa Uwanja wa Mkapa kwa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya APR kutoka Rwanda kitaumana kwa wababe hao ndani ya uwanja kusaka ushindi na utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliokuwa na kikosi hicho kwa msimu wa 2023/24.

Katika usajili Simba haijatikisa kwenye anga la Bongo kutokana na kuwa na wachezaji wenye majina ya kawaida tofauti na watani zao wa jadi Yanga ambao wao wanatarajia kutambulisha pia wachezaji wao na benchi la ufundi Agosti 4 2024.

Gumbo kubwa kwa Yanga ni Clatous Chama ambaye alikuwa ndani ya Simba msimu wa 2023/24 alifunga mabao 7 na pasi sita za mabao kibindoni.

Ni Mutale Joshua anatajwa kuwa moja ya mchezaji ambaye amefanya vizuri katika maandalizi kambini Misri akiwa ni moja ya wanaopewa nafasi kufanya vizuri.

Kambi ya Misri imegota mwisho na msafara wa Simba unatarajiwa kuanza kuwasili Bongo Julai 31 kwa maandalizi ya mwisho kuelekea Simba Day ambapo tiketi zake zinaendelea kuuzwa kwa sasa vituo mbalimbali.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa kazi kubwa itakuwa kwenye utambulisho huku mipango ikiwa inakwenda vizuri.

“Ni vizuri kila kitu kinakwenda Simba Day ni moto na kikosi kipo vizuri baada ya kuweka kambi nchini Misri tunaamini kwamba itakuwa ni siku nzuri na mashabiki wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Mkapa kushuhudia burudani ya kweli.”

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button