HomeKITAIFAMILIONI 500 KUWAPELEKA YANGA ROBO FAINALI

MILIONI 500 KUWAPELEKA YANGA ROBO FAINALI

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeweka mezani dau nono kama sehemu ya kuhamasisha kikosi kuelekea mchezo wao muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS FAR Rabat.

Mchezo huo wa marudiano unachezwa leo majira ya saa 4:00 usiku katika dimba la Olympique De Rabat lililopo jijini Rabat, Morocco, ukiwa na uzito mkubwa kwa hatma ya timu hiyo kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Inaelezwa kuwa mfadhili mkuu wa klabu hiyo, GSM, ameahidi kutoa kiasi cha Shilingi milioni 500 endapo Yanga itaibuka na ushindi katika pambano hilo la hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ahadi hiyo imekuja katika wakati muafaka ambapo Yanga inahitaji matokeo chanya ili kujihakikishia tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali, hatua ambayo itakuwa mafanikio makubwa kwa klabu hiyo katika safari yao ya kimataifa.

Ushindi dhidi ya AS FAR Rabat utakuwa na maana kubwa si tu kwenye msimamo wa kundi, bali pia katika kurejesha morali ya kikosi na kuonyesha ubora wa timu hiyo katika ushindani wa kimataifa.

Endapo Yanga itafanikiwa kupata ushindi, Shilingi milioni 500 hazitakuwa tu zawadi kwa wachezaji, bali pia ishara ya uwekezaji na dhamira ya dhati ya uongozi kuiona klabu ikivuka hatua zaidi na kuandika historia mpya barani Afrika.

Inaelezwa kuwa ahadi hiyo imepokelewa kwa furaha kubwa ndani ya kambi ya Yanga, huku wachezaji wakionekana kuwa na ari na dhamira ya kupambana hadi dakika ya mwisho ili kufikia malengo yao.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, kiungo wa Yanga, Pacome Zouzoua amesema kikosi kipo tayari kupigania nembo ya klabu hiyo na kuhakikisha kinapata matokeo chanya.

“Wachezaji wote tupo tayari kutimiza malengo yetu katika mchezo wa leo. Tutapambana kwa kiwango chetu bora ili kupata matokeo yatakayotupeleka hatua ya robo fainali,” amesema Pacome.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular