Arsenal Warejea Kileleni EPL Baada ya Ushindi Mwembamba Dhidi ya Everton

Arsenal

Arsenal wamerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL) kufuatia ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Everton katika dimba la Hill Dickinson, jijini Liverpool.

Bao pekee la mchezo lilifungwa dakika ya 27 na Viktor Gyökeres kwa mkwaju wa penalti, bao lililotosha kuwapa The Gunners alama zote tatu muhimu.

Kwa ushindi huo, Arsenal wamefikisha pointi 39 baada ya michezo 17, wakipanda hadi nafasi ya kwanza, alama mbili mbele ya Manchester City, ambao wameshuka hadi nafasi ya pili baada ya kukaa kileleni kwa muda mfupi.

Everton walijitahidi kusaka bao la kusawazisha hasa kipindi cha pili, lakini safu ya ulinzi ya Arsenal iliendelea kuwa imara na kuhakikisha wageni wanaondoka na ushindi.

Matokeo hayo yanaendeleza ushindani mkali kileleni mwa EPL huku mbio za ubingwa zikizidi kuchangamka.

FT: Everton 0-1 Arsenal
⚽ 27’ Gyökeres (P)