Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home ยป HII HAPA TAREHE YA MECHI YA SIMBA NA YANGA MWAKA HUU 2025
    KITAIFA

    HII HAPA TAREHE YA MECHI YA SIMBA NA YANGA MWAKA HUU 2025

    ChikaoBy ChikaoAugust 20, 202501 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    MECHI ya Simba na Yanga inatarajiwa kuchezwa mapema ikiwa ni ufunguzi wa msimu mpya wa 2025/26 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii (Community Shield) itakayowakutanisha Yanga SC na Simba SC, Septemba 16, 2025 jijini Dar.

    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa kwa mwaka huu, Ngao ya Jamii itachezwa kwa mchezo mmoja pekee kufuatia mabadiliko ya kanuni yaliyopitishwa na Kamati ya Utendaji. Awali, mashindano haya yalikuwa yakihusisha nusu fainali mbili na kisha fainali.

    Mabadiliko hayo yamesababishwa na msongamano wa ratiba, ikiwemo Tanzania kuwa mwenyeji wa Fainali za CHAN zitakazomalizika Agosti 30, pamoja na mechi mbili za mchujo za Kombe la Dunia zinazokabili Taifa Stars mapema Septemba. Mara baada ya Ngao ya Jamii, vilabu vya Tanzania vitakuwa vitani tena kwa michezo ya raundi ya awali ya mashindano ya CAF.

    Ipo wazi kwamba msimu wa 2024/25 Ngao ya Jamii ni Yanga SC ilitwaa ambapo ilichezwa kwa mfumo wa kuanzia hatua ya nusu fainali.

    Simba SC ilikuwa mshindi wa pili baada ya kucheza na Coastal Union ya Tanga huku Yanga SC ikitwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi mbele ya Azam FC.

    Simba SC Yanga SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleSIMBA KUFUNGWA KWENYE PRE SEASON NI FAIDA KUBWA KWA KOCHA FADLU
    Next Article SIMBA SC KUZINDUA UZI MPYA AGOSTI 27 2025

    Related Posts

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    March 24, 2026

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    March 24, 2026

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    March 24, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    Yanga Yamrudisha Kocha Abdihamid Moalin Kuinua Kiwango cha Timu

    Zidane Kurithi Mikoba ya Deschamps Ufaransa Baada ya Kombe la Dunia 2026

    Katibu wa Senegal asema Kombe halitaondoka Nchini kwao.

    FIFA YAPITISHA SHERIA MPYA 6 KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2026

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.