Home KITAIFA RAIS WA FIFA AMPONGEZA KARIA KWA KUREJEA TENA MADARAKANI

RAIS WA FIFA AMPONGEZA KARIA KWA KUREJEA TENA MADARAKANI

22
0

Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino ametuma salama za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa kuchaguliwa tena kuongoza nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka minne.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na TFF imesema Rais Infantino amempongeza pia Makamu wa Rais, pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa katika uchaguzi huo.

Aidha,Amemshukuru Rais Karia kwa juhudi, kazi na mchango wake muhimu katika maendeleo ya mpira wa miguu pamoja na kusimamia thamani yake na kumtakia heri na mafanikio.

Advertisement

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here