Home KITAIFA HUU HAPA UKWELI WA FADLU KUONDOKA SIMBA

HUU HAPA UKWELI WA FADLU KUONDOKA SIMBA

272
0
fadlu kuondoka simba

Mchambuzi nguli wa soka nchini, Saleh Jembe kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika taarifa kuhusiana na Kocha wa Klabu ya Simba, Fadlu David’s kuhusu kuondoka klabuni hapo.

“Hii ndio picha ya mwisho ya Kocha Fadlu David’s ambaye ameamua KUACHIA NGAZI SIMBA”

“Taarifa zinaeleza aligoma hata kupanda ndege kwenda Botswana”

“Alipigiwa simu na MO (Dewji) akamsihi asifanye hivyo, ndio akapanda ndege na kufika huko KATANGAZA KUACHANA NA Simba,” kilieleza chanzo, ameandika Saleh Jembe.

Je, Simba wataweza kumbakisha Fadlu David’s Msimbazi?

Mpaka sasa bado hakuna taarifa rasmi za kutoka ndani ya klabu ya simba juu ya ukweli wa taarifa hiyo hivyo tuendelee kusubiri na kupitia Sokaleo utapata habari hiyo kwa uharaka pindi tu ikifahamika ukweli wake.

BONYEZA HAPA KU DOWNLOAD NYIMBO MPYA ZA GOSPEL KILA SIKU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here