Manchester City wanafikiria namna ya kuuteka nyara uhamisho wa Chelsea wa kumnunua winga wa RB Leipzig wa Uholanzi Xavi Simons, 22. (Sport)
Brighton watahitaji zaidi ya pauni milioni 100 kwa Carlos Baleba baada ya Manchester United kuonyesha nia ya kumnunua kiungo huyo wa kati wa Cameroon mwenye umri wa miaka 21. (Telegraph – subscription required)
Mshambulizi wa Denmark Rasmus Hojlund yuko tayari kuondoka Manchester United msimu huu wa joto huku AC Milan ikijaribu kufanya mazungumzo ya mkataba wa mkopo na chaguo la kununua. (Gazzetta dello Sport – In Italian)
Manchester City wamemuongeza Maghnes Akliouche wa Monaco kwenye orodha ya wanaolengwa na watachuana na Bayer Leverkusen katika kuinasa saini ya winga huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23. (Florian Plettenberg)
Roma wapo kwenye mazungumzo na Aston Villa kuhusu kumnunua Leon Bailey lakini bado hawajawasilisha ombi rasmi kwa winga huyo wa Jamaica, 28, ambaye pia anazivutia klabu za Besiktas na Saudi Pro League. (Subscription required)
Fulham wako tayari kuvunja rekodi yao ya uhamisho ya £34m ili kumsajili winga wa Shakhtar Donetsk mwenye umri wa miaka 22 kutoka Brazil Kevin. (Sky Sports)
Manchester United wanatarajia Chelsea kuwasilisha ombi kwa Alejandro Garnacho, lakini The Blues wanatumai kumpata winga huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 21 kwa bei ya chini zaidi ya bei inayotakiwa na United ya £50m. (Sky Sports)
Southampton wametoa ofa ya pili kwa Everton kwa Tyler Dibling baada ya kukataa ofa tatu kutoka kwa Toffees kwa winga huyo wa chini ya miaka 21 wa England mwenye umri wa miaka 19. (Florian Plettenberg )
Nice wanaendeleza mazungumzo na Crystal Palace kuhusu kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Odsonne Edouard, 27. (Footmercato – in French)
Bayern Munich wametoa pauni milioni 52, nyongeza na sehemu ya mauzo yoyote kwa mshambuliaji wa Ujerumani Nick Woltemade, lakini Stuttgart wanadai pauni milioni 65. (Sky Sports in Germany)