HomeKITAIFAMPANZU AWASILI KAMBINI MISRI, AKABIDHIWA VIFAA VYAKE

MPANZU AWASILI KAMBINI MISRI, AKABIDHIWA VIFAA VYAKE

ELLIE Mpanzu, winga chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids amewasili kambini rasmi Agosti 5 2025 kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26.

Nyota huyo alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za watani wa jadi wa Simba SC ambao ni Yanga SC kuelekea msimu mpya wa 2025/26.

Inaelezwa kuwa alichelewa kambini kutokana na matatizo ya kifamilia jambo ambalo lilimfanya akachelewa kujiunga na Simba SC kambini nchini Misri.

Tayari kikosi cha Simba SC kimeanza maandalizi mapema kabla ya ligi kuanza. Ligi inatarajiwa kuanza kushika kasi Septemba 16 2025 ikiwa ni mwanzo wa msimu mpya.

Baada ya kuripoti kambini, Mpanzu amekabidhiwa vifaa vya kazi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya na alipata muda kuwasilimia wachezaji wa timu hiyo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Recent Comments

Web Development Company in Kochi,Kerala on NEYMAR AMWAGA MACHOZI AKIKUTANA NA KIPIGO KIKUBWA ZAIDI KWAKE