Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » KOCHA FADLU DAVIDS AFICHUA HESABU KUELEKEA MSIMU MPYA
    KITAIFA

    KOCHA FADLU DAVIDS AFICHUA HESABU KUELEKEA MSIMU MPYA

    ChikaoBy ChikaoAugust 10, 202502 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    fadlu simba
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    KOCHA Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids amesema kuwa wamefanya maboresho makubwa kwenye kikosi kwa kupata saini za wachezaji ambao watakuwa na kazi kupambana kwenye mashindano ambayo watashiriki.
    Simba SC msimu wa 2024/25 ilishiriki Kombe la Shirikisho Afrika na kugotea hatua ya fainali ikiwa nafasi ya pili na bingwa alikuwa RS Berkane.

    Msimu wa 2025/26 Simba SC itapeperusha bendera kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Fadlu ameweka wazi kuwa watakuwa kwenye aina tofauti ya mashindano ambayo yanahitaji ushindani mkubwa na aina ya wachezaji waliopo watakuwa na kazi kupambania ushindi.

    “Unaona kuna wachezaji ambao wamesaini kwenye kikosi. Ni aina ya wachezaji wazuri ni saini nzuri ambazo zipo kwenye kikosi. Tutakuwa kwenye mashindano tofauti msimu huu ukiachana na ligi tutakuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

    “Aina ya ushindani kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ni tofauti na kwenye Kombe la Shirikisho Afrika hivyo muhimu ni kuwa imara na tayari kwa ajili ya ushindani kwenye mechi zetu ambazo tutacheza.

    “Kambi ambayo ipo kwa sasa ninaona tunaendelea vizuri kuna mechi ambazo tutacheza kwa ajili ya kuwa imara zaidi hivyo bado tuna muda wakufanya maandalizi zaidi.”

    Miongoni mwa wachezaji wapya ambao wamesajiliwa Simba SC ni Jonathan Sowah mshambuliaji aliyekuwa Singida Black Stars, Abrahm Morice, beki wa kushoto Anthony Mligo aliyekuwa ndani ya Namungo FC.

    Simba SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleViktor Gyokeres ni mchezaji ‘Special’ – Ronaldo
    Next Article HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO TAREHE 11-08-2025

    Related Posts

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    March 24, 2026

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    March 24, 2026

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    March 24, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    Yanga Yamrudisha Kocha Abdihamid Moalin Kuinua Kiwango cha Timu

    Zidane Kurithi Mikoba ya Deschamps Ufaransa Baada ya Kombe la Dunia 2026

    Katibu wa Senegal asema Kombe halitaondoka Nchini kwao.

    FIFA YAPITISHA SHERIA MPYA 6 KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2026

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.