Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » YANGA SC NA HAIER FAMILIA, BILIONI 3.3 KUVUNWA
    KITAIFA

    YANGA SC NA HAIER FAMILIA, BILIONI 3.3 KUVUNWA

    ChikaoBy ChikaoAugust 7, 202502 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    YANGA SC itavuna kiasi cha shilingi bilioni 3.3 kutokana na kuongeza mahusiano na kampuni ya Haier wakisaini mkataba wa miaka mitatu rasmi Agosti 7 2025 katika Hotel ya Hyatt Regency, Dar.

    Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said amesema kuwa wana matumaini makubwa na mkataba huo kuwa ni faida kwa pande zote mbili kutokana na ukubwa wa Yanga SC na ubora wa bidhaa kutoka Haier.

    “Uhusiano wa Haier na Yanga SC ulikuwa na baraka kubwa. Ni matumaini yetu kuwa mkataba huu mpya utakuja na mafanikio zaidi. Msimu wa kwanza na Haier tulifika fainali ya Shirikisho Afrika. Mkataba huu utakuwa wa miaka mitatu mpaka mwaka 2028.

    “Uwepo wao kwa mara nyingine unatupa taswira kwamba tutakuwa na matokeo mengine mazuri kwa msimu mpya. Lakini safari hii tumeanza kwanza na ligi yetu ya ndani bado kutakuwa na mazungumzo mengine.

    “Nembo za Haier zitakaa mkono wa kushoto kwenye mashindano ya ligi. Mkataba huu utakuwa na thamani ya Tsh bilion 3.3.

    “Leo ni moja ya siku ya kihistoria kwa Klabu yetu. Leo tunatangaza kuongeza mahusiano na Haier hii ni taarifa njema sana kwa klabu yetu kwenye uimara wa kiuchumi wa timu yetu.

    “Mkataba wa awali ulikuwa mzuri sana. Tulifanya vyema sana kwenye mashindano ya shirikisho ambapo tulifika fainali. Kumbuka hiyo ilikuwa ni kwa mara ya kwanza tunaingia nao mkataba,”.

    Kwa upande wa Ibrahim Kiongozi ambaye ni Meneja wa Kampuni ya Haier Tanzania ameweka wazi kuwa mahusiano ya kampuni hiyo na Yanga SC yameleta mapinduzi makubwa kwenye soko.

    “Haier ni kampuni ya vifaa vya kieletroniki vya majumbani kutoka China. Mahusiano ya Haier, Yanga SC na GSM Group na yameleta mapinduzi makubwa.

    “Leo tumekuja kutangaza kuwa tunaendelea na mahusiano ambayo yamekuwa na manufaa kwa pande zote tatu.”

    Leon Chi Mkurugenzi wa Kanda Afrika Mashariki Haier amesema: “Nimejivunia kuwa sehemu ya watu ambao wamewezesha mahusiano baina ya Haier, GSM na Young Africans SC.

    “Nawashukuru sana Yanga SC kwa mchango wao mkubwa kwenye kutangaza bidhaa za Haier na nembo yetu kiujumla. Ni matarajio yetu mahusiano haya yatadumu na kuwa na tija kwa siku zijazo.”

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleBALEBA ATAKA KUJIUNGA NA MANCHESTER UNITED
    Next Article KOCHA SIMBA SC FADLU DAVIDS AFICHUA HESABU KUELEKEA MSIMU MPYA

    Related Posts

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    March 24, 2026

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    March 24, 2026

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    March 24, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    Yanga Yamrudisha Kocha Abdihamid Moalin Kuinua Kiwango cha Timu

    Zidane Kurithi Mikoba ya Deschamps Ufaransa Baada ya Kombe la Dunia 2026

    Katibu wa Senegal asema Kombe halitaondoka Nchini kwao.

    FIFA YAPITISHA SHERIA MPYA 6 KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2026

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.