Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » KOCHA WA YANGA HAELEWI, VIONGOZI WABADILISHA UELEKEO
    KITAIFA

    KOCHA WA YANGA HAELEWI, VIONGOZI WABADILISHA UELEKEO

    ChikaoBy ChikaoMarch 25, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    kocha wa yanga
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    UONGOZI wa klabu ya Yanga chini ya Rais wake, Hersi Said, umeonekana kumuweka katika wakati mgumu Kocha Mkuu, Pedro Goncalves, baada ya kumsisitiza kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji ambao kwa sasa hawapati muda wa kucheza.

    Hatua hiyo inatajwa kama aina ya “mtego” kwa kocha huyo, kwani inalazimika kubadili maamuzi yake ya kiufundi ili kuwajumuisha nyota ambao awali hawakuwa sehemu ya chaguo lake la kwanza.

    Mashabiki wa Yanga nao wamekuwa wakijiuliza kuhusu hatma ya baadhi ya wachezaji waliosajiliwa lakini hawapati nafasi ya kucheza, akiwemo Farid Mussa na Salum Aboubakar, jambo lililozua mjadala mkubwa ndani na nje ya klabu hiyo.

    Akizungumzia suala hilo, msemaji wa Yanga, Ali Kamwe, amesema kuwa katika kikao maalum kilichofanyika, kocha huyo aliwasilisha ripoti yake ya kiufundi na kuulizwa kuhusu sababu za kuwanyima nafasi baadhi ya wachezaji, huku viongozi wakiridhika na maelezo yake.

    Hata hivyo, viongozi hao wamesisitiza kuwa  umuhimu wa kila mchezaji kupata nafasi ya kuchangia uwanjani, wakiamini kuwa hata wale wenye mchango mdogo wanaweza kuongeza thamani yao iwapo watapewa muda wa kucheza.

    Kamwe amesema  msukumo huo unatokana na wingi wa michuano inayokabili klabu hiyo kwa sasa, ikiwemo Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho na michuano mingine, hali inayofanya kuwa muhimu kwa kikosi chote kushiriki kikamilifu.

    Ameongeza kuwa mashabiki wanapaswa kuwa na subira, akisisitiza kuwa wachezaji waliokuwa wakikosa nafasi wataanza kuonekana zaidi uwanjani mara baada ya timu kurejea kwenye ratiba ya ligi.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleHII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA
    Next Article TETESI: TIMU YA MESSI YAMFUKUZIA BERNARDO SILVA

    Related Posts

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    March 24, 2026

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    March 24, 2026

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    March 24, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    TETESI: TIMU YA MESSI YAMFUKUZIA BERNARDO SILVA

    KOCHA WA YANGA HAELEWI, VIONGOZI WABADILISHA UELEKEO

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    Yanga Yamrudisha Kocha Abdihamid Moalin Kuinua Kiwango cha Timu

    Zidane Kurithi Mikoba ya Deschamps Ufaransa Baada ya Kombe la Dunia 2026

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.