HomeKITAIFAAZAM WAMEPANIA KUPELEKA MOTO KWA WYDAD

AZAM WAMEPANIA KUPELEKA MOTO KWA WYDAD

Kikosi cha wachezaji 25 cha Azam FC kimesafiri leo asubuhi kuelekea Morocco kwa ajili ya mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wydad Athletic Club, utakaochezwa Jumapili.

Mchezo huo una umuhimu mkubwa kwa timu zote, huku ukiwa ndio utakaoamua hatma ya Azam FC katika safari yao ya mashindano hayo msimu huu.

Kwa sasa Azam FC ipo nafasi ya tatu kwenye kundi ikiwa na pointi tisa, idadi inayolingana na Maniema Union ya DR Congo, wakati Wydad Athletic Club wanaongoza kundi kwa pointi 12.

Pamoja na changamoto ya ushindani mkali, Kocha Mkuu Florent Ibenge amesisitiza kuwa kikosi chake bado kina matumaini na kipo tayari kupigania matokeo chanya katika mchezo huo muhimu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular