Miaka 3 baada ya kuuzwa Everton, James Garner kurejea Man U

James Garner Old

Manchester United wanaripotiwa kujaribu kumrejesha James Garner Old Trafford ikiwa ni miaka mitatu tu baada ya kumuuza Everton.
Kikosi cha Amorim kimekuwa na uhitaji wa kiungo mpya na nyota huyo ameonekna kuwa chaguo namba moja na la bei nafuu kuelekea dirisha la usajili la Januari.
Miaka mitatu iliyopita Man United walimuuza Garner kwa Everton kwa pauni milioni 9 ambapo mkataba wake na klabu hiyo utamalizika msimu ujao wa joto.