Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda amesema amepigiwa simu na Watanzania mbalimbali ambao wameahidi kutoa Shilingi Milioni 100 kwa kila goli watakalofunga Taifa Stars siku ya leo dhidi ya Uganda na ile ya Tunisia Desemba 30 katika mashindano ya Afcon yanayoendelea nchini Moroco.
Makonda amesema hayo alipokuwa akizungumza na wachezaji na benchi la ufundi la Stars kuelekea mchezo wao dhidi ya Uganda utakaochezwa siku ya leo katika dimba la Al Madina majira ya saa 2;30 usiku.
“Kuwathibitisha kuwa Watanzania wako pamoja na nyinyi, juzi na jana nimepokea simu za Watanzania ninaowaamini na kuwaheshimu wameniambia nenda kawaambia vijana wa Taifa Stars tupo nao na kuanzia mechi ya Uganda na Tunisia Watanzania wananunua goli moja Sh100 milioni,” amesema Makonda.
Taifa Stars inakutana na Uganda na Tunisia, baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Nigeria kwa bao 2-1 mchezo uliochezwa Desemba 23, 2025.










Leave a Reply