Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » MWENDO WA KIMYA KIMYA AISEE…SIMBA WASHUSHA MASHINE HII MPYA YA KAZI DAR….
    KITAIFA

    MWENDO WA KIMYA KIMYA AISEE…SIMBA WASHUSHA MASHINE HII MPYA YA KAZI DAR….

    ChikaoBy ChikaoOctober 15, 202502 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    simba
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    MABORESHO ya benchi la ufundi la Simba yanaendelea, baada ya ujio wa Dimitir Pantev na msaidizi wake, Simeonov Boyko Kamenov waliotokea Gaborone United ya Botswana, sasa ameshushwa mtu mwingine.

    Simba SC imemshusha kwa siri sana kocha wa makipa kutoka Bulgaria kwa ajili ya kuimarisha benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Dimitir Pantev.

    Mtaalamu huyo aliyetua majira ya saa 9:05 alfajiri na ndege ya Shirika la Uturuki, ni Vitomir Vutov mwenye umri wa miaka 53 ambapo amekuja kuungana na wenzake siku chache baada ya kuondoka kwa Fadlu Davids.

    Ujio wa Vutov, unalifanya benchi la ufundi la Simba kuwa na raia watatu kutoka Bulgaria, wengine ni Pantev aliyetambulishwa kama Meneja Mkuu na msaidizi wake, Simeonov Boyko Kamenov.

    “Ni kweli jamaa amekuja na leo (juzi) asubuhi amefika uwanja wa mazoezi kutambulishwa kwa wachezaji,” kimesema chanzo kutoka Simba.

    “Amekuja kwa ajili ya kuwafundisha makipa kwa sababu nafasi hiyo haikuwa na kocha baada ya Fadlu kuondoka na wasaidizi wake.”

    Hata hivyo, Simba inafanya siri sana juu ya ujio wa kocha huyo huku ikielezwa muda wowote atatambulishwa.

    Vutov ambaye rekodi zinaonyesha mara ya mwisho alikuwa na kikosi cha FC Lovech huko Bulgaria, anakuja kuchukua nafasi ya Wayne Sandilands ambaye ameondoka na Fadlu kuelekea Raja Casablanca.

    Rekodi zinaonyesha Vutov kabla ya kutua Simba, amepita kufundisha klabu kadhaa ikiwemo Spartak Varna, PFC Lokomotiv Plovdiv, FC Lokomotiv Gorna Oryahovitsa, Litex Lovech zote za Bulgaria.

    Septemba 22, 2025, wakati Fadlu anaaga ndani ya Simba, aliondoka na wasaidizi wake wanne ambao ni Darian Wilken (Kocha Msaidizi), Wayn Sandilands (Kocha wa Makipa), Durell Butler (Kocha wa Utimamu) na Mueez Kajee (Mchambuzi wa Video).

    Kuondoka kwa Fadlu na wasaidizi wake, imeifanya Simba kuboresha benchi la ufundi ambapo sasa Seleman Matola aliyeendelea kubaki kama kocha msaidizi, Pantev amekuja na msaidizi wake mwingine aliyekuwa naye Gaborone United. Pia Vutov ametua kwa ajili ya kuwanoa makipa, huku kocha wa utimamu akipewa jukumu hilo amepewa mzawa, Mohamed Mrishona Mohamed ‘Xavi’.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleUWANJA WA SOKOINE WAFUNGIWA KUCHEZWA MECHI ZA LIGI KUU
    Next Article SIMBA JOTO LAPAMBA MOTO KUELEKEA MECHI DHIDI YA NSINGIZINI

    Related Posts

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    March 24, 2026

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    March 24, 2026

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    March 24, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    Yanga Yamrudisha Kocha Abdihamid Moalin Kuinua Kiwango cha Timu

    Zidane Kurithi Mikoba ya Deschamps Ufaransa Baada ya Kombe la Dunia 2026

    Katibu wa Senegal asema Kombe halitaondoka Nchini kwao.

    FIFA YAPITISHA SHERIA MPYA 6 KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2026

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.