Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » TAKWIMU ZA KELVIN JOHN HUKO DENMARK
    KIMATAIFA

    TAKWIMU ZA KELVIN JOHN HUKO DENMARK

    ChikaoBy ChikaoSeptember 29, 202501 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    kelvin john
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    Mshambuliaji wa AaB Fodbold ya Denmark, Kelvin John licha ya timu yake hiyo kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Lyngby Boldklub amezidi kuwa bora na amesema huu ni msimu wake wa kuonyesha kiwango bora.

    Juzi, timu ya Mtanzania huyo ilipoteza mabao 2-1 dhidi ya Lyngby Boldklub kwenye muendelezo wa Ligi Daraja la Kwanza Denmark na licha ya kufungwa, John alionyesha kiwango bora kwa kufunga bao moja ambalo linamfanya kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mechi, kura zinazopigwa na mashabiki.

    Bao alilofunga linamfanya kufikisha jumla ya mabao sita kwenye mechi 10 alizocheza. Timu hiyo ipo nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi baada ya kukusanya pointi 14.

    Akizungumza na AaB TV, John alisema huu ni msimu wake wa kufanya vizuri, kuonyesha kiwango bora na kuwa na muendelezo wa kufunga. “Ninapofunga kila mechi inanipa ujasiri wa kuendelea kufunga, hivyo huu ni msimu wangu wa kufanya vizuri na kuisaidia timu yangu imalize nafasi nzuri,” alisema John

    Huu ni msimu wa pili kwa John kuitumikia timu hiyo ambayo msimu uliopita ilimaliza mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu Denmark na kushushwa daraja, hivyo sasa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleUKWELI WA ISHU YA YANGA KUACHANA NA KOCHA FOLZ
    Next Article FIFA YAIADHIBU AFRIKA KUSINI KWA KUMCHEZESHA MCHEZAJI ASIYE NA SIFA

    Related Posts

    Zidane Kurithi Mikoba ya Deschamps Ufaransa Baada ya Kombe la Dunia 2026

    March 24, 2026

    Katibu wa Senegal asema Kombe halitaondoka Nchini kwao.

    March 20, 2026

    RICHARLISON SHUJAA WA TOTTENHAM VS LIVERPOOL, WAIPINGIZA MAKALI

    March 16, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    Yanga Yamrudisha Kocha Abdihamid Moalin Kuinua Kiwango cha Timu

    Zidane Kurithi Mikoba ya Deschamps Ufaransa Baada ya Kombe la Dunia 2026

    Katibu wa Senegal asema Kombe halitaondoka Nchini kwao.

    FIFA YAPITISHA SHERIA MPYA 6 KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2026

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.