Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » BERNARD MORRISON ATOA SHUKRANI KWA WALIOSIMAMA NAYE KATIKA SAFARI YA KUPONA MAJERAHA YA GOTI
    KITAIFA

    BERNARD MORRISON ATOA SHUKRANI KWA WALIOSIMAMA NAYE KATIKA SAFARI YA KUPONA MAJERAHA YA GOTI

    ChikaoBy ChikaoJuly 6, 202502 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Morrison
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    Mchezaji wa soka wa kimataifa kutoka Ghana, Bernard Morrison, ametoa andiko la kugusa moyo kupitia ukurasa wake rasmi, akieleza safari yake ya mateso kutokana na jeraha la goti ambalo lilimweka nje ya uwanja kwa karibu mwaka mmoja. Katika andiko hilo, Morrison amewashukuru watu mbalimbali waliomsaidia katika kipindi hicho kigumu cha maisha yake ya soka na kuweza kumrudisha uwanjani.

    Morrison alianza kwa kueleza kuwa tangu mwezi Januari 2024, aliporejea Tanzania kwa ajili ya matibabu ya goti lake, alikumbana na changamoto nyingi, ikiwemo ukosefu wa huduma sahihi na ucheleweshwaji wa matibabu sahihi, hali iliyosababisha kuendelea kwa maumivu kwa muda mrefu.

    Baada ya vipimo vya MRI, aligundulika kuwa na tatizo kubwa la “Meniscus Grade 3 Tear”, lakini daktari aliyemfanyia upasuaji wa awali hakulishughulikia ipasavyo. Morrison aliuita upasuaji huo kuwa wa “kipuuzi” na kusema daktari huyo alitumia goti lake kama “mechi ya kirafiki”.

    Hata hivyo, kupitia msaada wa watu wachache wenye nia njema, Morrison aliweza kusimama tena. Akiwataja kwa majina, Morrison amesema:

    🟢 “Mheshimiwa Hamis Mwinjuma (Mwana FA) alionyesha upendo na kujali kwa kunisaidia kuunganishwa na watu waliowezesha matibabu, akiwemo Mr. Ndama na Mr. Kitumbo wa Tabora United.”

    🟢 “Mr. Salim Abdallah ‘Try Again’ alilipia gharama ya upasuaji, akiwa miongoni mwa waliohakikisha nimepata huduma bora. Martin Arthur (Kofi Kinaata) naye alichangia gharama ya upasuaji.”

    🟢 “Daktari Edwin Kagabo na physiotherapist Hamisi Kimweri walinipa matumaini, tiba na msaada mkubwa bila hata kuwa na mkataba wowote nami.”

    🟢 “Mr. Kenneth, mmiliki wa KenGold SC, ndiye aliyenipa nafasi ya pili ya kurejea uwanjani – nafasi ambayo leo inanifanya nicheze tena mpira wa ushindani.”

    Morrison alieleza pia kuwa licha ya maumivu yaliyoendelea hata baada ya upasuaji, alijitahidi kuvumilia na kufanya mazoezi kwa bidii hadi alipoanza tena mazoezi ya mpira mwezi Machi 2025.

    “Sijui ningekuwaje leo kama si nyinyi,” alisema Morrison kwa hisia kubwa, akihitimisha kwa kusema:
    “Asante sana. Mungu awabariki nyote kwa wema wenu. Niko tena uwanjani kwa sababu ya upendo wenu.”

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleENG. HERSI SAID AENDELEA KUIBEBA SOKA LA AFRIKA KUPITIA ACA
    Next Article BABA MZAZI WA MBWANA SAMATTA AFARIKI DUNIA

    Related Posts

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    March 24, 2026

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    March 24, 2026

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    March 24, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    Yanga Yamrudisha Kocha Abdihamid Moalin Kuinua Kiwango cha Timu

    Zidane Kurithi Mikoba ya Deschamps Ufaransa Baada ya Kombe la Dunia 2026

    Katibu wa Senegal asema Kombe halitaondoka Nchini kwao.

    FIFA YAPITISHA SHERIA MPYA 6 KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2026

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.