Author: Chikao

Kiungo wa kati wa Croatia, Luka Modric, amemtaja Bernardo Silva kama mchezaji mwingine wa Ureno anayempenda mbali na Cristiano Ronaldo. Nahodha huyo wa Real Madrid ameyasema hayo kabla ya mechi ya Kundi A ya Ligi ya Mataifa ya Croatia dhidi ya Ureno itayopigwa usiku wa leo Alhamisi mjini Lisbon. “Kwenye kikosi cha Ureno, kando na Cristiano Ronaldo, Bernardo Silva ndiye mchezaji mwingine ninayempenda” alisema Modric.

Read More

Jana tumecheza mechi yetu ya mazoezi pale KMC na tumesikia milio Mingi ikivuma, tuwaambie ule ni uwanja wa Halmashauri ya Kinondoni ni fedha zetu wanakinondoni tumejenga ule uwanja, KMC tumempa tu ausimamie. “Sasa wewe uwanja sio wako unaongea ongea tumefuata nini, wewe ni kwako? Na ule uwanja unapataje heshima kama Yanga haendi pale, watu wa mwenge jana wamefurahi sana kutuona sasa kama imewauma hameni na tutakuja tena, we unaumia kwako pale, sisi tunacheza popote hata bunju tukitaka tutacheza” Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga Sc, Ally Kamwe.

Read More

BAADA ya timu ya taifa ya Tanzania , Taifa Stars kutoshana nguvu na timu ya taifa ya Ethiopia katika mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2025 Hemed Morocco, Kaimu Kocha Mkuu wa Stars amesema kuwa wamecheza na tim ngumu hivyo haikuwa rahisi kupata matokeo mazuri. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa Septemba 4 2024 umesoma Tanzania 0-0 Ethiopia hivyo hakuna aliyeibuka na ushindi kwenye mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa. Katika dakika 45 za mwanzo timu zote mbili hakuna ambayo ilipiga shuti lililolenga lango huku kipindi cha pili katika dakika za lala salama wachezaji wa Tanzania walifanya majaribio yaliyokuwa na hatari ikiwa…

Read More

BAADA ya Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids kuchaguliwa kuwa kocha bora ndani ya Agosti 2024 na Jean Ahoua kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Agosti, uongozi wa Simba umetoa ufafanuzi kuwa kwa namna yoyote ile ilikuwa ni lazima watwae tuzo hiyo kutokana na rekodi zilizoandikwa. Ipo wazi kuwa baada ya mechi mbili msimu wa 2024/25 Simba imekusanya pointi 6 ndani ya dakika 180 safu ya ushambuliaji ikifunga mabao saba. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema: “Mnaonalalamika tuzo ya mwezi zimetolewaje wakati wengine wana mechi moja wengine wana mechi mbili tufanye wote tumecheza mechi moja bado…

Read More

Kocha wa timu ya Taifa Uholanzi Ronald Koeman amesema wazi kuwa ameacha kumuita mchezaji wake nyota wa timu ya taifa ya Uholanzi Steven Bergwijn kwasababu ameondoka kwenye ligi ya Uholanzi na kujiunga na klabu ya Al Ittihad ya ligi ya Saudia. “Kama una miaka 26 kitu muhimu zaidi n kucheza siyo pesa. angebaki tu Ajax wanalipa vizuri pia, kwa umri wake hakupaswa kufanya uamuzi kama ule. nimefunga mlango wake wa kuichezea timu ya Taifa ya Uholanzi” alisema Koeman. Steven Bergwijn mwenye umri wa miaka 26 hadi sasa ameichezea Uholanzi michezo 35 akiwa na magoli 8.

Read More

Baada ya Soka Leo kuripoti juu ya taarifa za Aliyewahi kuwa mchezaji wa Simba, beki wa kulia Israel Mwenda, ambaye tulieleza kwamba amepanga kufikisha malalamiko yake FIFA. Sasa kuna habari mpya kumhusu mchezji huyo aliyesajiliwa na Singida Black Stars, awali alikuwa ameongezewa mkataba na Simba lakini aliomba kutafuta changamoto mpya, na ndipo Simba wakamruhusu akaondoka, huku nafasi yake akizida Kelvin Kijili aliyetokea Singida Big Stars pia. Israel Mwenda amesema kwamba Stimu yake ya sasa, imevunja makubaliano ya kimkata na yeye hana pa kwenda kwa sasa, kwani dirisha la usajili limekwisha fungwa. “Nipo kwenye mchakato wa kuvunja mkataba, nyie subirini mtapata…

Read More

BENCHI la ufundi la timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars limeweka wazi kuwa maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Ethiopia yapo vizuri kwa kila mchezaji kuwa tayari kuipambania jezi ya Tanzania. Ni Septemba 4 2024 Taifa Stars inatarajiwa kushuka Uwanja wa Mkapa kwa ajili ya mchezo huo wa kuwania kufuzu AFCON 2025 itakuwa ni saa 1:00 usiku. Juma Mgunda, Kocha msaidizi wa Taifa Stars amesema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri kwa wachezaji kuwa tayari kuelekea mchezo huo dhidi ya Ethiopia. “Kuhusu mchezo wetu dhidi ya Ethiopia maandalizi yako vizuri ninaweza kusema kuwa kwa zaidi ya asilimia 80 yamefikia tunaendelea kujiandaa ili kupata matokeo…

Read More

Baada ya mfululizo wa matokeo mabaya tangu kuanza kwa msimu wa ligi kuu Uingereza 2024-25 Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Manchester United Omar Berrada amesema utawala wa timu hiyo una imani kubwa na kocha mkuu wa timu hiyo Erik Ten Hag ambaye amekuwa akipondwa sana na mashabiki wa timu hiyo. “Tunafikiri Erik Ten Hag ndiye kocha sahihi kwetu na tunamuunga mkono kikamilifu kwa 100%” alisema Berrada ambaye ni C.E.O wa Manchester United baada ya kipigo cha 3-0 kutoka kwa Liverpool. Uongozi wa timu hiyo chini ya kampuni ya INEOS iliyo chini ya tajiri wa Uingereza Sir Jim Ractliffe umeendelea…

Read More