HomeKITAIFASingida Black Stars yaituliza Mtibwa Sugar

Singida Black Stars yaituliza Mtibwa Sugar

MTIBWA Sugar 1-3 Singida Black Stars, (SBS) ni matokeo rasmi mchezo wa NBC Premier League uliochezwa mapema leo Februari 22,2026 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Wageni Singida Black Stars wamewatuliza wenyeji kwenye mchezo wa leo ambao ulichezwa saa 8:00 mchana katika msako wa pointi tatu muhimu.

Magoli ya SBS yamefungwa na Ndumumwe Mossi dakika ya 5, Horso Malanga dakika ya 16 na Kennedy Juma dakika ya 58.

Goli pekee la wenyeji Mtibwa Sugar limefungwa na Raizin Hafidhi dakika ya 89. Pointi tatu zimechukuliwa na mgeni.

Mara baada ya mchezo huo Horso alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo akikabidhiwa zawadi na wadhani wa ligi NBC.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular