Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » “Xavi ameumia wachezaji wale wale Hans Flick anashinda”Laporta.
    KIMATAIFA

    “Xavi ameumia wachezaji wale wale Hans Flick anashinda”Laporta.

    ChikaoBy ChikaoMarch 10, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    Mgombea urais wa Barcelona, Joan Laporta, amefunguka kuhusu kauli zilizotolewa na Xavi Hernández katika mahojiano yake na La Vanguardia akisema Xavi anaumizwa na mafanikio ya Hans Flick anayoyapata akiwa na wachezaji wale wale aliokuwa nao Xavi.

    Kiungo huyo wa zamani na kocha aliushambulia vikali uongozi wa zamani, akimlaumu Laporta kwa kushindikana kurejea kwa Lionel Messi mwaka 2023, huku pia akidai kuwa mshirika wa karibu wa Laporta, Alejandro Echevarria, ndiye anayeendesha mambo ndani ya klabu.

    Laporta ameweka wazi kuwa ameumizwa na kauli za Xavi na akasisitiza kuwa uamuzi wake wa kuachana na kocha huyo wa zamani ulikuwa sahihi.

    “Nilishangaa na kuumia. Ninapoona kauli hizi kutoka kwa Xavi, namfikiria Hansi Flick. Ni vigumu kuwa rais wa Barça na lazima uchukue maamuzi magumu nilifanya kile nilichopaswa kufanya,”

    “Kwa Xavi, niliona kwamba tulikuwa tunaenda kupoteza, na kwa Flick ninaona kwamba tutaenda kushinda ninaelewa kwamba ameumia kwa wachezaji wale wale, Xavi alikuwa anapoteza, na Flick anashinda.”

    “Haya ni maamuzi matatu magumu zaidi niliyowahi kufanya: Lionel Messi, Ronald Koeman na Xavi Hernández. Niliyafanya nikiweka maslahi ya Barça mbele. Wawili kati yao nilikuwa nao kama wachezaji, lakini haya ni maamuzi ambayo lazima yafanywe. Wote ni magwiji wa Barça”.

    “Barça haiwezi kuendeshwa kwa kutumia kompyuta tu; ni suala la hisia. Barça iko juu ya wachezaji na hata marais.” Amesema Laporta.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleKAGOMA ASEMA BADO ANA KAZI KUBWA SIMBA
    Next Article Barcelona Inaweza Kuwa na Kipaumbele Kumchukua Erling Haaland

    Related Posts

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    April 7, 2026

    MBAPPE: NITACHEZEA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON

    April 4, 2026

    TETESI: TIMU YA MESSI YAMFUKUZIA BERNARDO SILVA

    March 25, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    MBAPPE: NITACHEZEA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.