Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » TUMEFUATA SHERIA, HAKUNA KURUKA HATUA. MANGUNGU
    KITAIFA

    TUMEFUATA SHERIA, HAKUNA KURUKA HATUA. MANGUNGU

    ChikaoBy ChikaoFebruary 19, 202601 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    MWENYEKITI wa Simba, Muhtaza Mangungu, amesema uongozi wa klabu hiyo umepokea rasmi maboresho ya Katiba kutoka Serikalini na tayari umeanza kuyafanyia kazi kwa kuzingatia taratibu na sheria za nchi.

    Kauli hiyo imekuja kufuatia hatua ya Msajili wa Vyama vya Michezo kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuikabidhi Simba Katiba yao iliyofanyiwa marekebisho, huku wakisisitiza klabu kuendelea na mchakato huo kama ilivyoelekezwa.

    Mangungu ameeleza kuwa uongozi umepokea maelekezo hayo na unahitaji muda wa kuyapitia na kuyatekeleza kwa umakini, ili kuhakikisha kila kipengele kinafanyiwa kazi kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa ndani ya Katiba hiyo pamoja na miongozo ya kisheria.

    Amesisitiza kuwa mchakato wa mabadiliko ndani ya klabu si jambo dogo, kwani unagusa mamlaka zaidi ya moja za Serikali, hali inayohitaji umakini na uratibu wa kina.

    “Kuna eneo linalosimamiwa na Wizara ya Michezo, kuna eneo linalosimamiwa na Wizara ya Katiba na Sheria, pia  linalosimamiwa na Wizara ya Viwanda na Biashara,” amesema Mangungu, akibainisha kuwa kila hatua lazima izingatie matakwa ya kisheria.

    Ameongeza kuwa mchakato huo ulianza muda mrefu, hivyo utekelezaji wake unahitaji subira na kufuata taratibu zote za kisheria ili kuhakikisha mageuzi hayo yanafanyika kwa usahihi na kwa manufaa ya klabu pamoja na wanachama wake.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleTFF Yafungua Zabuni ya Haki za Kipekee za Ubashiri Dabi ya Kariakoo
    Next Article Barcelona Yatakiwa Kulipa Pauni 26M Kumng’oa Rashford Manchester United

    Related Posts

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    April 12, 2026

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    April 8, 2026

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.