Home KITAIFA SIMBA WATUMA SALAMU KALI, JINA LA MPINZANI HALINA MAANA

SIMBA WATUMA SALAMU KALI, JINA LA MPINZANI HALINA MAANA

0
72

KIUNGO wa Simba SC, Innocent Loemba amesema kwa sasa kikosi chao hakitazami majina ya wapinzani wanaokutana nao, bali kimeweka nguvu zote katika kusaka ushindi na alama tatu muhimu katika kila mchezo wanaocheza.

Nyota huyo ameeleza kuwa ushindani ndani ya ligi umekuwa mkubwa kwa kila timu, hali inayowalazimu wachezaji wa Simba kuingia uwanjani wakiwa na ari kubwa ya kupambana ili kuhakikisha wanaitetea nembo ya klabu yao kwa nguvu zote.

Loemba amesema kuwa kwa sasa wachezaji wamekubaliana kuweka pembeni majina makubwa au madogo ya wapinzani wao, kwa sababu wanatambua kuwa kila timu inayokutana nao inakuwa na malengo yake ya kupata matokeo mazuri.

Amesisitiza kuwa kila mchezo kwao ni muhimu na haupaswi kubezwa, kwani timu nyingi zimekuwa zikionyesha ushindani mkubwa pindi zinapokutana na Simba, jambo linalowafanya wao kuongeza umakini zaidi ndani ya uwanja.

“Hakuna mechi iliyorahisi kwetu, hatuangalii timu tunakutana nayo iwe Singida Black Stars au Pamba Jiji FC, kikubwa ni kuingia kwa nguvu, mshikamano na kupambana kutafuta alama tatu ili kufikia malengo yetu,” amesema Loemba.

Kiungo huyo ameweka wazi kuwa ushindani uliopo ndani ya kikosi cha Simba kwa sasa ni mkubwa, jambo linalowafanya wachezaji kujituma zaidi kila wanapopata nafasi ya kucheza ili kusaidia timu kupata matokeo chanya.

Loemba ameongeza kuwa nguvu kubwa wanayoipata inatokana na mashabiki wa Simba ambao wamekuwa wakiisapoti timu hiyo kila wanapocheza, jambo linalowapa hamasa wachezaji kupambana zaidi ili kuendelea kuwapa furaha mashabiki hao kila wanapopata nafasi ya kushuka dimbani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here