KIMATAIFA

TAJIRI WA UNITED AFUTA MKATABA WA FERGUSON

MMILIKI mwenza wa Manchester United kampuni ya Ineos inayomilikiwa na bilionea Sir Jim Ratcliffe imesitisha mkataba wa mamilioni wa Sir Alex Ferguson kuwa balozi wa klabu hiyo.

Ferguson, 82, aling’atuka kwenye kiti cha ukocha wa Man United mwaka 2013 kabla ya kusaini mkataba mpya wa kuwa balozi wa timu hiyo.

Na kilichoelezwa ni kwamba kwenye mkataba huo, Ferguson aliripotiwa kulipwa zaidi ya Pauni 2 milioni (Sh 7bilioni) kwa mwaka tangu Oktoba 2013, lakini sasa mkataba huo unaripotiwa kusitishwa na Ineos.

Ferguson aliambiwa ana kwa ana kwenye mkutano wake na bilionea Sir Jim Ratcliffe, ambaye kwa sasa anapambana kupunguza gharama za uendeshaji kwenye kikosi hicho msimu huu na kwamba Ferguson hataendelea kulipwa zaidi ya msimu huu.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button