Ruka hadi maudhui
SOKALEO

Neymar JR acheza na kutupia licha ya kuwa na jeraha la goti.

Chikao
Neymar JR acheza na kutupia licha ya kuwa na jeraha la goti.

Nyota wa Timu ya Taifa ya Brazil na klabu ya Santos Neymar Jr siku ya jana alifanya maamuzi ya kucheza mchezo muhimu wa klabu yake wa vita ya kujinusuru kushuka daraja licha ya jeraha la goti alilonalo ambalo alitakiwa kufanyiwa upasuaji.

Neymar Jr siku kadhaa zilizopita aliripotiwa kupata jeraha jipya la goti ambalo madaktari walishauri afanyiwe upasuaji licha ya ripoti hiyo nyota huyo alifanya maamuzi ya kucheza mchezo wa Santos dhidi ya Sport akiisaidia kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 baada ya kufunga bao na kutoa pasi ya bao huku akiimbwa na mashabiki wa timu yake.

Baada ya mchezo huo Neymar ameahidi kuwa atakuwepo pia kwenye mchezo ujao kwani jeraha hilo si kitu cha kumzuia.

“Jeraha hili ni la kusikitisha, la kuudhi lakini si kitu kitakachonizuia. Nitakuwepo kwenye mchezo ujao pia.”Amesema Neymar Jr.

Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →

Vigogo wa Ulaya Kukipiga Leo Kwenye UEFA

Dani Carvajal aondoka Madrid baada ya miaka 23

MICHAEL OWEN: Ni mapema mno kumfukuza Carrick Manchester United

Kunyoa kumenipa faragha mtaani, watu hawanitambui – Haaland