Kiwiko dhidi ya Anthony Mligo champonza Mayanga afungiwa mechi 5.

mayanga

Mchezaji wa Mbeya City, Vitalis Mayanga amefungiwa kucheza mechi tano sambamba na kutozwa faini ya Tsh Milioni 1 kwa kosa la kumpiga kiwiko beki wa kushoto wa Simba, Anthony Mligo kwenye mchezo wa ligi kuu uliopigwa katika dimba la Meja Isymuhyo disemba 4 mwaka huu.

Uamuzi huo umetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) katika taarifa ya TPLB siku ya leo kwa mujibu wa kanuni ya 41;21 ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa wachezaji.