Mchezaji wa zamani wa Yanga anayekipiga klabu ya Wydad kwa sasa Stephane Aziz Ki ameandika ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa Instagram akimtakia kila la kheri mke wake mwanamitindo wa Tanzania Hamisa Mobetto katika kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.
Aziz Ki ambaye alifunga ndoa na mwanamitindo huyo wa Tanzania mapema mwaka huu kwa sasa anakipiga Nchini Morocco huku mpaka sasa wakiwa bado hawajajaliwa kupata mtoto pamoj licha ya kila mmoja kuwa na watoto nje ya ndoa yao.
“Mpenzi wangu Hamisamobetto,
Katika siku hii maalum, nataka nikukumbushe umuhimu wako maishani mwangu. Kila mwaka nikiwa pembeni yako ni zawadi ya thamani—sura mpya iliyojaa mapenzi, furaha, na kumbukumbu zisizosahaulika.
Wewe ni nguvu yangu, upole wangu, amani yangu, na msukumo wangu. Kwa sababu yako mimi ni mwanaume bora, na kila muda ninaokuona hunikumbusha jinsi nilivyo barikiwa kukupenda na kupendwa na wewe.
Leo, siadhimishii tu siku yako ya kuzaliwa… ninaadhimisha mwanamke wa kipekee uliye: moyo wako mkarimu, tabasamu lako la faraja, ujasiri wako, nuru yako, na namna uwepo wako unavyoangaza maisha yangu.
Naomba mwaka huu mpya wa maisha yako uje na furaha zaidi, mafanikio, amani, na upendo. Na ujue kwamba daima nitakuwa hapa kando yako—kukupenda, kukusaidia, na kukuthamini jinsi unavyostahili.
Heri ya Siku ya Kuzaliwa, malkia wangu.
Nakupenda zaidi ya maneno yanavyoweza kuelezea,
MIRS KI”Ameandika Azizi Ki.










Leave a Reply