Mechi dhidi ya Man City kuamua hatma ya Alonso Real Madrid.

Man City kuamua Alonso

Real Madrid walizomewa walipolala kwa mabao 2-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Celta Vigo katika mechi waliyomaliza wakiwa na wachezaji tisa.

Celta walikuwa mkiani mwa La Liga kabla ya safari yao ya Bernabeu Jumapili usiku na bila ushindi wa ligi dhidi ya Real Madrid katika mechi 22.

Lakini mabao ya Williot Swedberg kipindi cha pili yalihitimisha ushindi wa kwanza wa Celta dhidi ya Madrid tangu Mei 2014 na kuongeza shinikizo kwa kocha Xabi Alonso.
Real Madrid sasa wameshinda mchezo mmoja tu kati ya michezo mitano iliyopita ya ligi na watashuka hadi nafasi ya tatu kwenye La Liga iwapo Villarreal watashinda mchezo wao mkononi.
Gazeti la Uhispania AS linasema pambano la Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City Jumatano linaonekana likatoa taswira’ kwa Real Madrid na Alonso kwani hawatarajii kupoteza kwa Celta Vigo kuathiri ‘mustakhbali wake wa hivi karibuni’ katika kazi hiyo.