Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA
    KITAIFA

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    ChikaoBy ChikaoApril 5, 202601 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Ibenge
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    KOCHA Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, amesema kikosi chake kinafahamu vizuri ubora wa Simba, huku akisisitiza kuwa mchezo wao wa leo utakuwa na hadhi ya kimataifa kutokana na uzoefu wa timu zote mbili kwenye michuano ya Afrika.

    Azam FC itakuwa mwenyeji wa pambano hilo dhidi ya Simba, litakalopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam, ambapo mashabiki wanatarajia kushuhudia ushindani mkali.

    Ibenge ameeleza kuwa Simba si timu ndogo, na ndio maana wanauchukulia mchezo huo kwa uzito mkubwa, akiuona kama mechi yenye ladha ya kimataifa kutokana na historia ya hivi karibuni ya timu hizo katika mashindano ya Afrika.

    Amefafanua kuwa Simba ilishiriki hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Azam FC nayo ilifika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, jambo linaloonyesha ubora wa pande zote mbili.

    “Hautakuwa mchezo rahisi hata kidogo. Tunautambua ubora na ukubwa wa Simba, lakini sisi pia tupo tayari kupambana. Hii ni mechi yenye hadhi ya Afrika,” amesema Ibenge.

    Azam FC Simba SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleMBAPPE: NITACHEZEA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON
    Next Article MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    Related Posts

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    April 19, 2026

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    April 19, 2026

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    April 19, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    SINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.