Nahodha wa Manchester City, Bernardo Silva (31), rasmi ameagwa na klabu hiyo kufuatia kumalizika kwa mkataba wake, akihitimisha safari yake ya kihistoria jijini Manchester.
Silva, aliyejiunga na City akitokea AS Monaco mwaka 2017, ameacha alama kubwa baada ya kucheza zaidi ya mechi 450 na kuchangia mafanikio ya mataji 15 makubwa, yakiwemo ya msimu wa kihistoria wa Treble (2022/23). Kiungo huyo mbunifu pia aliwahi kukabidhiwa unahodha kufuatia kuondoka kwa Kevin De Bruyne, jukumu alilolitekeleza kwa weledi mkubwa chini ya kocha Pep Guardiola.
Kuondoka kwake sasa kunahitimisha rasmi enzi ya mmoja wa viungo bora kuwahi kuitumikia City, huku mashabiki wa City wakimpa heshima ya mwisho kwa mchango wake mkubwa ndani ya klabu hiyo.
