AZAM YAMLETA HAALAND BONGO, ANA BALAA HATARI

azam
Klabu ya Azam FC imetangaza rasmi kukamilisha usajili wa mshambuliaji chipukizi, Aimar Hafidh Abubakar, maarufu kama ‘Haaland’, akitokea klabu ya Mlandege FC ya Zanzibar katika dirisha hili la usajili la Januari 2026.
Usajili wa mchezaji huyo, ambaye amejizolea umaarufu kutokana na uwezo wake wa kufumania nyavu, unatajwa kuwa ni sehemu ya mkakati wa “Tajiri wa Jiji” kuimarisha safu yao ya ushambuliaji baada ya kufanya vizuri na kuiondosha Simba SC katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Kwa kuingia kwa Aimar Hafidh, Azam FC inaendeleza falsafa yake ya kusaka vipaji bora kutoka kanda ya Afrika Mashariki.