Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » ONYO LA MAPEMA, YANGA YAREJEA KILELENI KWA KISHINDO
    KITAIFA

    ONYO LA MAPEMA, YANGA YAREJEA KILELENI KWA KISHINDO

    ChikaoBy ChikaoFebruary 26, 202601 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    KLABU  ya Yanga imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliopigwa kwa ushindani mkubwa.l katika dimba la KMC Complex uliopo Mwenge Dar es Salaam.

    Katika pambano hilo, Yanga ilionyesha ubora mkubwa kuanzia dakika za mwanzo hadi mwisho wa mchezo, ikitawala umiliki wa mpira na kutengeneza nafasi nyingi za mabao.

    Ushindi huo umeipa timu hiyo morali kubwa kuelekea michezo ijayo, hususan Kariakoo Derby inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki.

    Mabao ya Yanga yalifungwa na Mohamed Hussein, Laurindo Dilson ‘Depu’, Mudathir Yahya, Prince Dube na Sheikhan Khamis, kila mmoja akichangia kwa namna yake kuifanya timu hiyo iondoke na alama zote tatu muhimu.

    Kwa matokeo hayo, Yanga imefikisha pointi 28 na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi sawa na JKT Tanzania waliopo nafasi ya pili. Hata hivyo, Yanga inaongoza kutokana na ubora wa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

    Ushindi huo si tu umeimarisha nafasi yao juu ya msimamo, bali pia umetuma salamu nzito kwa wapinzani wao kabla ya Kariakoo Derby, huku kikosi hicho kikionekana kuwa katika kiwango bora na tayari kwa mapambano makubwa yanayofuata.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleKikosi cha Simba vs Dodoma Jiji Leo 25/02/2026
    Next Article Yanga Yatuma Salamu Msimbazi Baada ya Ushindi wa 5-0 Dhidi ya JKT Tanzania

    Related Posts

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    April 12, 2026

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    April 8, 2026

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.