Nimeona baadhi ya mashabiki wa kandanda wakimtupia maneno ya kejeli beki wa kimataifa wa Ivory Karaboue Chamou anayeichezea klabu ya Simba kwa sasa.
Mashabiki wengi wanamfuata na kumzodoa beki huyo kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya Simba kupoteza mchezo wowote.
Haya yote sababu yake nini? Na kwanini inakuwa hivyo.
Kiufundi Karaboue Chamou ni beki mwenye nidhamu ya hali ya juu katika uchezaji wake. Ni beki tafu sana kama utaamua kwenda nae hewani au kufanya naye battle.
Namkumbuka Karaboue Chamou aliyeifikisha Simba Hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu uliopita mara baada ya Che Malone Fondoh kuumia na kuonekana kiwango chake kimedorora. What A Performance.
Karaboue Chamou ni mchezaji mzuri saana lakini anakosa sifa moja ya speed pale ambapo anakutana na washambuliaji wenye speed kali.
Simba mnaye beki mzuri endeleeni kumtia moyo ndiye beki a Simba kwa sasa aliye active.










Leave a Reply