Ruka hadi maudhui
SOKALEO

Steve Barker Afunguka Sababu za Simba Kufanya Makosa ya Kujenga Mashambulizi Nyuma

Chikao
Steve Barker Afunguka Sababu za Simba Kufanya Makosa ya Kujenga Mashambulizi Nyuma

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amewatoa hofu mashabiki na wadau wa soka akieleza kuwa hana presha yoyote kutokana na makosa yanayofanywa na wachezaji wake wakati wa kuanzisha mashambulizi kutoka eneo la ulinzi.

Akizungumza baada ya ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya 15 de Agosto ya Equatorial Guinea kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Barker alisisitiza kuwa mtindo huo ni sehemu ya falsafa yake ya kudumu ya uchezaji.

Licha ya kukiri kuwa kujenga mashambulizi kuanzia nyuma kuna hatari zake—hasa pale mpira unapopotea katika eneo la hatari na kuwapa wapinzani nafasi—kocha huyo alieleza kuwa timu inapaswa kuvumilia changamoto hizo badala ya kuachana na mfumo huo.

“Hilo halinipi presha. Tunacheza kwa mtindo unaohusisha kujenga mashambulizi kuanzia nyuma, na katika mfumo huo makosa ya aina hiyo yanaweza kutokea,” alieleza Barker.

Aliongeza kuwa wakati mwingine mambo yanaweza yasiende kama walivyopanga uwanjani, lakini jambo la msingi ni wachezaji kuendelea kuwa waaminifu kwa falsafa ya benchi la ufundi na kujifunza kupitia makosa hayo.

Ushindi huo wa mabao 6-1 unaiweka Simba SC katika nafasi nzuri sana kuelekea mchezo wa marudiano, huku Barker akiweka wazi dhamira yake ya kuendelea kuimarisha timu bila kuondoa mfumo wake wa asili wa kucheza mpira wa kuvutia.

Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →