Ruka hadi maudhui
SOKALEO

Baada ya Doumbua Kutupia, Hans aibuka Asema "Humu Hamna Mshamguliaji"

Chikao
Baada ya Doumbua Kutupia, Hans aibuka Asema "Humu Hamna Mshamguliaji"

Mchambuzi wa michezo kutoka kituo cha habari cha Crown FM, Hans Rafael, ametoa mtazamo wake mkali kuhusu mshambuliaji wa Simba SC, Doumbia, huku akionesha mashaka makubwa juu ya uwezo na aina ya mchezaji huyo kikosini hapo.

​Hans Rafael kupitia maoni yake amebainisha kuwa atakuwa mtu wa mwisho kuamini kama Doumbia ndiye aina ya mshambuliaji anayestahili kuchezea klabu hiyo ya Msimbazi, akisisitiza kuwa Simba SC bado inahitaji mshambuliaji namba 9 aliye bora zaidi yake.

​Mchambuzi huyo amehitimisha mtazamo wake kwa msemo wa dhihaka kuwa hata saa mbovu kuna siku inasema ukweli, akimaanisha kuwa ingawa mchezaji huyo anaweza kufunga au kufanya vizuri mara moja moja, hiyo haiondoi ukweli kwamba klabu hiyo inahitaji mshambuliaji wa kiwango cha juu zaidi.

Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →