Ruka hadi maudhui
SOKALEO

Hili la kocha limeshaisha - Ali Kamwe

Chikao
Hili la kocha limeshaisha - Ali Kamwe

Baada ya Yanga kuachana na kocha wao Manqoba Mngqithi, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa timu hiyo Ali Kamwe amesema suala hilo limeshaisha.

Yanga imeachana na kocha huyo raia wa Afrika Kusini baada ya kumalizika kwa pambano lao na TRA United lililofanyika Arusha. 

Kupitia ukurasa wake rasmi Ali Kamwe ameandika kuwa “La Kocha limeshapita. Manqoba hayupo tena. Kwa sasa tuwape muda uongozi wetu ufanye tathmini ya nani anakuja kuchukua nafasi hiyo."

Kamwe aliendelea;

“Lakini wakati hilo likiendelea na Ligi pia inaendelea. JUMANNE, Yani (kesho) tu hapo tuna mechi ya nyumbani dhidi ya Mashujaa pale uwanja KMC Complex. Hatuwezi kundelea kuangusha pointi mfululizo. Hili Halikubaliki.

“Jumanne tuje tuungane na Players wetu kutafuta Pointi 3 muhimu. Wanayanga wenzangu hii ni mechi Yetu na Players wetu

wanatuhitaji sana. Tufanye tufanyavyo, Jumanne tuungane pamoja, sisi na Players wetu Tuutafute ushindi wetu In Shaa Allah” ameandika Kamwe.

Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →