Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR
    KIMATAIFA

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    ChikaoBy ChikaoApril 17, 202601 Min Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email
    Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Misri (EFA) limewasimamisha kazi kwa muda usiojulikana mwamuzi na wasaidizi wake waliohusika katika mchezo wa daraja la pili kati ya Tanta na Telecom Egypt, kufuatia kitendo cha ajabu cha kutumia simu ya mkononi kama “VAR ya mchongo”. Katika hali iliyozua mshangao, mwamuzi huyo alionekana akitumia simu ya mmoja wa watu waliokuwa karibu na uwanja kupitia upya picha za video za tukio la penalti iliyokuwa na utata. Baada ya kujiridhisha kupitia kioo cha simu hiyo, mwamuzi huyo aliamua kufuta maamuzi ya awali ya penalti, jambo ambalo ni kinyume kabisa na taratibu za mpira wa miguu duniani.
    ​Tukio hilo limetajwa kama moja ya matukio ya ajabu zaidi kuwahi kushuhudiwa katika soka la Afrika, likizua mjadala mzito kuhusu matumizi ya teknolojia uwanjani. Shirikisho la Misri tayari limeanzisha uchunguzi wa kina kubaini simu hiyo ilikuwa ya nani na jinsi ilivyofika mikononi mwa mwamuzi katikati ya mchezo. Wakati wachambuzi wa soka wakicheka na kusema “soka la Afrika halichoshi”, mamlaka za soka nchini Misri zimechukua hatua hiyo ya dharura kulinda hadhi ya mchezo huo, huku zikisisitiza kuwa matumizi ya teknolojia lazima yafuate kanuni rasmi za FIFA na CAF.
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleSINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC
    Next Article KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    Related Posts

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    April 16, 2026

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    April 7, 2026

    MBAPPE: NITACHEZEA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON

    April 4, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    SINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC

    BERNARDO AAGWA NA MAN CITY RASMI

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.