aada ya uwepo wa tetesi kuhusu Yanga kumuhitaji Selemani Mwalimu Klabu ya Young Africans SC (Yanga) imekanusha taarifa hizo kuhusu kuvutiwa na mshambuliaji wa Simba SC, Selemani Mwalimu, na kuweka wazi kuwa hakuna mazungumzo yoyote yanayoendelea kati yao na mchezaji huyo.
Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram, Afisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, alieleza kuwa taarifa hizo si za kweli bali ni uzushi unaolenga kutumia jina la Yanga kwa maslahi binafsi ya mawakala. Alisisitiza kuwa uongozi wa klabu haujawahi kufanya mawasiliano na upande wowote kuhusu kumsajili Mwalimu, na kutoa wito kwa mawakala kubuni njia nyingine halali za kuwatafutia wachezaji wao mikataba badala ya kulitumia jina la Yanga.
